Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane huenda akakaa nje kwa wiki sita
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane huenda akakaa nje kwa hadi wiki sita baada ya kupata jeraha la misumi ya paja akichezea Senegal mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Mchezaji huyo
hataweza kucheza dhidi ya Manchester United na Tottenham na pia mechi mbili za
Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Maribor.
Mane, 25, aliondolewa
uwanjani dakika ya 89 mechi ambayo walilaza Cape Verde 2-0 Jumamosi.
Mane amefunga mabao
matatu katika mechi tano za Ligi ya Premia alizocheza msimu huu.
Liverpool walishinda
mechi moja pekee kati ya saba katika mashindano yote Mane akiwa michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari.
Senegal, wanaongoza
kundi lao la kufuzu kwa Kombe la Dunia, lakini wana mechi muhimu dhidi ya
Afrika Kusini mnamo 10 na 14 Novemba, mechi ambazo kuna uwezekano huenda Mane
akakosa kushiriki.
Mabao ya wastani
waliyofunga wakiwa na Mane Ligi ya Premia ni 2.2, na bila yeye 1.6 kila mechi.
No comments