Baada ya tetesi nyingi kumuhusu mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho kuhamia Barcelona, sasa sio tetesi tena bali ni rasmi mchezaji huyo amejiunga na mabingwa hao wa Hispania.
Coutinho amejiunga na Barcelona kwa dau la Euro milioni €160 na tayari ametua nchini Hispania kwa ajili ya vipimo.
Coutinho (25) amesaini mkataba wa miaka mitano na nusu ambao unadhani ya Euro milioni 400 na leo jumapili atakuwa uwanjani kuishuhudia timu yake mpya ya Barcelona ikiivaana na Levante katika mchezo wa Ligi kuu nchini humo (La Liga).
Hadi kuhama kwake, Coutinho akiwa Liverpool amecheza mechi 201 na kuifungia magoli 54, na alijiunga na Liverpool akitokea Inter Millan kwa dau la Euro milioni €8.5 .
Kwa mujibu wa mtandao wa Klabu ya Barcelona umesema kuwa kesho jumatatu mchezaji huyo ataungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi .
No comments